• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Harry Kane alenga kufikia rekodi za Shearer na Rooney kwa magoli katika EPL

    (GMT+08:00) 2020-06-25 16:09:20

    Mshambuliaji matata wa Tottenham Hotspur, Harry Kane amesema kwamba analenga kuwa mchezaji wa tatu baada ya Alan Shearer na Wayne Rooney kufunga jumla ya mabao 200 katika Ligi Kuu ya Uingereza (EPL). Jumatatu wiki hii, Kane alifunga goli katika ushindi wa 2-0 wa Tottenham dhidi ya West Ham United katika kipute cha EPL, na kuwa bao lake la 137 katika jumla ya mechi 200 ambazo amewachezea Tottenham. Hadi kufikia sasa, ni Shearer pekee na Rooney ndio wanajivunia kupachika wavuni zaidi ya mabao 200 katika historia ya soka ya EPL. Kwa sasa, Sergio Aguero wa Manchester City ndiye anayejivunia idadi kubwa zaidi ya mabao katika soka ya Uingereza, akiwa amefunga magoli 138, moja zaidi ya Kane.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako