• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Idadi ya maambukizi ya virusi vya Corona barani Afrika yazidi laki 3.2

    (GMT+08:00) 2020-06-25 17:06:08

    Takwimu kutoka Kituo cha Kukinga na Kudhibiti Magonjwa Afrika (Africa CDC) zimeonyesha kuwa, idadi ya jumla ya kesi zilizothibitishwa kuwa na maambukizi ya virusi vya Corona barani Afrika imefikia 326,236, na idadi ya jumla ya vifo imefikia 8,642, na wagonjwa 154,877 wamepona.

    Nchi inayoongoza kwa idadi kubwa zaidi ya maambukizi ni Afrika Kusini, ambayo mpaka kufikia jana ilikuwa na kesi zaidi ya laki moja zilizothibitishwa kuwa na virusi vya Corona. Waziri wa fedha wa nchi hiyo Tito Mboweni amesema kutokana na athari ya maambukizi ya virusi vya Corona, uchumi wa Afrika Kusini utapungua kwa asilimia 7.2.

    Naibu waziri wa afya wa Kenya Bibi Mercy Mwangangi amesema, asilimia 78 ya wagonjwa hawana dalili au wana dalili ndogo, hali inayowezesha utekelezaji wa kuwapatia matibabu wakiwa nyumbani. Amesema kwa sasa haiwezekani tena kwa miji ya Nairobi na Mombasa, ambayo inabeba mzigo mkubwa, kuwatenga wagonjwa katika hospitali.

    Tume ya Kuratibu mapambano dhidi ya virusi vya Corona nchini Mali hivi karibuni imesema, ingawa idadi ya maambukizi imepungua, lakini haionyeshi Mali imepata ushindi katika vita dhidi ya virusi vya Corona. Ili kuhakikisha mwelekeo mzuri wa hali ya maambukizi nchini humo, mashirika ya afya ya Mali yatafanya upimaji wa virusi vya Corona kwa watu wengi mjini Bamako. Aidha kamati ya sayansi ya Mali imekubali kuanzisha tena shughuli za mashindano ya michezo, lakini wahusika wanatakiwa kufanyiwa upimaji saa 72 kabla ya mashindano, na watazamani hawaruhusiwi kwenda viwanjani.

    Nchini Cape Verde, serikali imetangaza kuwa kutokana na kuendelea kwa kesi za maambukizi ya virusi vya Corona, serikali haitarejesha safari za ndege za kimataifa kabla ya mwezi Agosti. Awali, serikali hiyo ilitangaza kurejesha safari za ndege za kimataifa mwezi Julai, ili kuunga mkono sekta ya utalii.

    Ikulu ya Senegal imetoa taarifa ikisema, rais Macky Sall jana aliwasiliana kwa karibu na mtu mmoja aliyethibitishwa kuambukizwa virusi vya Corona, na amejitenga kwa siku 15.

    Aidha, idara ya takwimu ya Msumbiji wiki hii imeanza uchunguzi wa kote nchini kwa wiki mbili, ili kuthibitisha athari ya maambukizi ya virusi vya Corona kwa viwanda nchini humo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako