• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Maonesho ya 127 ya biashara ya China kwa kupitia mtandao wa Internet ni ishara chanya ya China katika kupanua ufunguaji mlango

  (GMT+08:00) 2020-06-25 19:29:38

  Maonesho ya 127 ya biashara ya kimataifa ya China yaliyofanyika kwa siku 10 mjini Guangzhou yamemalizika jana.

  Hii ni mara ya kwanza kwa maonesho hayo kufanyika kwa njia video katika miaka 60 iliyopita. Kampuni elfu 26 kutoka ndani na nje ya China zilishiriki, na wafanyabiashara kutoka nchi na sehemu 21 duniani walijiandikisha kwenye maonesho hayo, bidhaa milioni 1.8 zilioneshwa kupitia mtandao wa Internet, na maelfu ya studio elfu yalitangaza maonesho hayo kupitia mtandao wa Internet. Kufanyika kwa maonesho hayo kwa kupitia mtandao wa Internet kumeonesha ishara chanya ya China katika kupanua ufunguaji mlango, na uwajibikaji wa China katika kufanya juhudi za kulinda usalama wa mnyonyoro wa uzalishaji na utoaji wa huduma duniani, hatua ambayo imechochea imani ya soko la dunia.

  Hayo ni maonesho ya kimataifa ya biashara yenye historia ndefu zaidi tena ni makubwa zaidi nchini China, na yanasifiwa kuwa ni ishara muhimu ya biashara na nje ya China, na ni alama muhimu ya China katika kufungua mlango nje.

  Wateja wa maonesho hayo wanatoka nchi na sehemu mbalimbali duniani, hali ambayo imeonesha umuhimu mkubwa wakati uchumi wa dunia unapodorora kutokana na janga la virusi vya Corona, huku biashara na uwekezaji wa kimataifa zinaposhuka kwa kiasi kikubwa. Ripoti kuhusu Takwimu na Makadirio kuhusu biashara ya kimataifa iliyotolewa tarehe 23 na Shirika la Biashara duniani WTO imeonesha kuwa, katika robo ya kwanza ya mwaka huu, thamani ya biashara ya mizigo duniani ilishuka kwa asilimia 3 kuliko mwaka jana wakati kama huu, na inakadiriwa kuwa, kiasi hicho kitaendelea kupungua na kufikia asilimia 18.5 katika robo ya pili ya mwaka huu. Ni wazi kuwa, maonesho hayo yameleta uhai kwa uchumi na biashara duniani.

  China ikiwa nchi kubwa zaidi kutokana na biashara ya mizigo duniani, hatua yake ya kuimarisha biashara na nje itakuwa nguzo katika kutuliza biashara na uchumi wa dunia.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako