• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wakulima wa miwa wakaribisha Sheria ya Jumla ya Mazao ya 2020

    (GMT+08:00) 2020-06-26 08:19:40

    Wakulima wa miwa wamekaribisha Sheria ya Jumla ya Mazao ya 2020 iliyochapishwa kwa gazeti la serikali na waziri wa Kilimo Peter Munya, akisema sheria hiyo itachangia soko huru kwa bidhaa zao.

    Shirika la Kitaifa la Wakulima wa sukari ya Kenya (KNASFO) limesema hatua hizo mpya zitawawezesha kujihusisha na kilimo cha mikataba ambacho kitawaruhusu wakulima wa miwa kushiriki kwa minada mikubwa.

    Baadhi ya wakulima wamesema hatua hiyo itafufua uzalishaji mkubwa wa mazao katika maeneo ya miwa yaliyotelekezwa na pia kupunguza mapato duni kwa sekta hiyo.

    Wadau wa sukari kwenye ukanda wa Nyando unaojumuisha kaunti za Kisumu, Kericho na Nandi na pia Mkoa wa Magharibi ambao unajumuisha kaunti ya Bungoma, Kakamega, Busia na Vihiga wamekaribisha Sheria hiyo. Na kusema sasa mashamba ya miwa mbayo yalio kuwa yametekelezwa na wakulima wa miwa katika mikoa yote sasa litafufuliwa na kutumika.

    Chini ya kanuni mpya, mkataba wa usambazaji wa miwa itakuwa jambo kati ya muuzaji wa bidhaa kutoka shamba na msagaji wa chaguo lake, hakuna mtu wa tatu.

    Huu ni ushindi kwa wakulima ambao kwa muda mrefu walikuwa wamezuiliwa kwa viwanda visivyo fanya kazi, kupitia kugawa maeneo, na kupata hasara kubwa.

    Kanuni mpya itatoa uteuzi wa kamati ya wadau ambayo itaamua vigezo vya bei ya miwa ambayo itakuwa msingi wa ubora kando na ile ya uzito wa miwa.

    Hii ni njia moja ya kusaidia kufufua viwanda.

    Pia wameunga mkono hatua ya kukodisha viwanda vianvyomilkiwa na Serikali, ili kusaidia kufufua viwanda vyenye vinafanya vibaya.

    Wakulima wameshutumu kuongezeka kwa uagizaji wa sukari haramu nchini wakisema nchi inauwezo wa kuzalisha sukari yake bila kutegemea nchi zengine kwa bidhaa hiyo.

    Wamesema kufikia sasa bei ya sukari imeshuka kwa asilimia 21 na hii imeathiri sana wakulima wa miwa katika maeneo ya zao hilo. Wakati viwanda vya sukari vinanganga kupata soko la bidhaa zao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako