Mjumbe wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Balozi Zhang Jun, amesema China inaunga mkono mchakato shirikishi wa amani nchini Afghanistan, na iko tayari kutoa jukwaa la mazungumzo ya ndani kwa ajili ya Afghanistan. Serikali ya Afghanistan na Kundi la Taliban wameweka msingi kwa mazungumzo ya ndani kwa kubadilishana wafungwa. Bw. Zhang amesema China inapongeza hatua hii, na kutaka pande zote kufikia makubaliano kuhusu mipango ya mazungumzo ya ndani juu ya mwundo wa kisiasa wa nchi hiyo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |