• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Ni rasmi Liverpool ndio mabingwa wa EPL

    (GMT+08:00) 2020-06-26 18:43:17

    Liverpool walinyakua ubingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) kwa mara ya kwanza baada ya miaka 30 jana Juni 25 kufuatia ushindi wa 2-1 uliosajiliwa na Chelsea dhidi ya mabingwa watetezi Manchester City. Ushindi kwa Man-City uwanjani Stamford Bridge ungalichelewesha zaidi karamu ya Liverpool wanaofundishwa na kocha mzawa wa Ujerumani, Jurgen Klopp. Katika kipindi cha misimu miwili iliyopita ya EPL, Man-City walikuwa wamepoteza jumla ya michuano sita pekee na kutawazwa wafalme wa 2017-18 na 2018-19 kwa alama 100 na 98. Ingawa hivyo, kichapo kutoka kwa Chelsea, ambacho kilikuwa kichapo chao cha nane kupokea msimu huu, kiliwafanya kubaki na alama 23 zaidi nyuma ya Liverpool. Liverpool walitwaa rasmi ubingwa wa soka ya Uingereza msimu huu zikisalia mechi saba zaidi katika kampeni za kivumbi hicho.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako