• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uchumi wa utalii wa China waendelea kufufuka katika likizo ya sikukuu ya Duanwu

    (GMT+08:00) 2020-06-28 16:53:05

    Takwimu zilizotolewa na Wizara ya Utamaduni na Utalii ya China zimeonyesha kuwa, katika siku tatu za likizo ya sikukuu ya kijadi ya Duanwu, wachina milioni 48.809 walifanya utalii. Idadi hiyo ni asilimia 50.9 ya ile ya mwaka jana, na kuleta pato la utalii Yuan bilioni 12.28 (dola zaidi ya bilioni 1.7 za kimarekani) ambalo ni asilimia 31.2 ya mwaka jana.

    Kwa vile kimsingi uenezi wa virusi vya Corona nchini China umedhibitiwa, na maisha yameanza kurudi katika hali ya kawaida. Watu wengi waliamua kusafiri kwa kuendesha magari na kushiriki kwenye burudani zinazohusu mila na desturi za jadi katika sikukuu hiyo yenye historia zaidi ya 2,000. Hata hivyo watu wanachukua tahadhari na kufuata maelekezo ya wataalamu wa afya kama vile kuvaa barakoa. Vituko zaidi ya asilimia 90 vya utalii nchini China vimeanzisha mfumo wa kuagiza tiketi kwenye mtandao wa Internet ili kuepuka mkusanyiko mkubwa wa watu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako