• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China asisitiza kutanguliza wananchi kwanza katika kupambana na mafuriko na majanga ya kijiografia

    (GMT+08:00) 2020-06-29 09:10:21

    Rais Xi Jinping wa China ametoa wito wa kuongeza juhudi zaidi katika kuzuia, kuokoa na kazi za misaada kutokana na mafuriko na majanga ya kijiografia, na kutoa kipaumbele katika kuhakikisha maisha na usalama wa watu.

    Rais Xi ametoa maagizo hayo wakati China ikiingia katika msimu wa mvua, pia amepongeza juhudi zilizofanywa na serikali za mitaa, akisema matokeo chanya yameonekana katika kudhibiti mafuriko na katika kazi za uokoaji. Aidha, rais Xi amesisitiza umuhimu wa kuwatanguliza wananchi kwanza, na kuthamini maisha ya watu katika kukabiliana na mafuriko.

    Rais Xi amesema, wakati sehemu nyingi zinaingia kwenye msimu wa mafuriko, huku baadhi zikikabiliana na mazingira magumu, Makao Makuu ya Kudhibiti Mafuriko na Ukame pamoja na idara nyingine zinapaswa kuongeza uratibu na kutoa mwongozo katika kuzuia mafuriko na kimbunga.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako