• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yatoa punguzo kwa usafirishaji wa mizigo SGR

    (GMT+08:00) 2020-06-29 09:10:43

    Kampuni ya reli ya Kenya imetoa punguzo la bei kwa wateja wake wanaotumia huduma ya usafirishaji wa mizigo ya reli ya SGR.

    Kampuni hiyo imesema, bei ya kusafirisha kontena la futi 20 lililojaa kutoka Mombasa hadi ghala la makontena la ndani la Naivasha (ICD) itakuwa dola za Marekani 480, na bei ya kusafirisha kontena kuelekea bandari ya Mombasa itakuwa dola za Marekani 240. Pia usafirishaji wa kontena tupu kutoka Naivasha ICD hadi Mombasa utalipiwa ushuru wa dola za Marekani 120.

    Kampuni hiyo pia imesema, punguzo hilo jipya litaendelea mpaka tarehe 30, mwezi Agosti.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako