• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Viongozi wa Afrika Mashariki wampongeza rais mpya wa Malawi

    (GMT+08:00) 2020-06-29 09:30:12

    Viongozi wa nchi za Afrika Mashariki wametuma salamu za pongezi kwa rais mpya wa Malawi Lazarus Chakwera aliyeapishwa jana baada ya kushinda katika marudio ya uchaguzi mkuu.

    Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amesema ushindi wa Chakwera umethibitisha hamu ya wananchi wa Malawi ya kupata uongozi ambao utaunganisha na kuhimiza nchi yao ifikie kwenye kiwango kipya cha maendeleo.

    Rais Edgar Lungu wa Zambia kwa upande wake amesema ushindi wa Chakwera umathibitisha tena imani ambayo wananchi wa Malawi wanayo juu yake. Pia amesisitiza kuwa ataendelea kushirikiana kwa karibu na kiongozi huyo mpya wa Malawi kuendeleza urafiki wa jadi kati ya nchi hizo.

    Bw. Chakwera alimshinda aliyekuwa rais wa nchi hiyo Peter Mutharika kwa kupata asilimia 58.57 ya kura kwenye upigaji kura uliofanyika Jumanne, baada ya Mahakama ya Katiba ya nchi hiyo kufuta ushindi wa Mutharika katika uchaguzi uliofanyika mwezi Mei mwaka 2019 kutokana na kuwepo kwa vitendo vya udanganyifu katika uchaguzi huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako