• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania yatambulisha aina mpya za zabibu ili kuongeza uzalishaji wa divai

    (GMT+08:00) 2020-06-29 09:30:36

    Mkuu wa Kituo cha Makutopora cha Taasisi ya Utafiti wa Kilimo ya Tanzania TARI huko Dodoma Bw. Cornel Massawe amesema, aina 13 za zabibu kutoka Afrika Kusini zitatambulishwa ili kuongeza uzalishaji wa divai nchini humo.

    Bw. Massawe amesema ukosefu wa aina za zabibu ya divai umekwamisha uzalishaji wa divai nchini Tanzania, na kwamba aina hizo za zabibu kutoka Afrika Kusini pamoja na hatua nyingine mbalimbali zitasaidia kuongeza kilimo cha zabibu nchini humo, hatua inayotarajiwa kuchochea uzalishaji wa mvinyo.

    Takwimu kutoka Wizara ya Kilimo ya Tanzania zimeonesha kuwa, kuna wakulima 1,696 wa zabibu huko Dodoma, na jumla ya uzalishaji wa divai ni tani 10,052 kwa mwaka.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako