• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Maofisa wa Marekani waonya kuongezeka zaidi kwa maambukizi ya virusi vya Corona

  (GMT+08:00) 2020-06-29 18:27:11

  Takwimu kutoka Gazeti la New York Times la Marekani zinaonyesha kuwa, idadi ya maambukizi kote Marekani katika siku 14 zilizopita imeongezeka. Baada ya majimbo mbalimbali kuondoa zuio na kuanza tena shughuli za kazi na uzalishaji, idadi ya maambukizi ya virusi vya Corona imeongezeka tena, ambapo maofisa wengi wa Marekani wametoa onyo kutokana na hali hiyo.

  Tarehe 28, waziri wa afya na huduma za umma wa Marekani Bw. Alex Azar ameonya kuwa, dirisha la kudhibiti maambukizi ya virusi vya Corona nchini Marekani linafungwa, kila mtu anapaswa kuchukua hatua za kuwajibika. Watu wanapaswa kukaa mbali, kama wako katika mazingira yasiyowaruhusu kuwa mbali na mwingine, wanapaswa kuvaa barakoa, hasa katika sehemu zenye hali mbaya ya maambukizi.

  Mkuu wa jimbo la New York Andrew Cuomo pia ameonya kuwa, kama haikuchukuliwa hatua na kuruhusu maambukizi ya virusi vya Corona kuongezeka zaidi, Marekani itakabiliwa na msukosuko mkubwa wa taifa.

  Aliyekuwa mkurugenzi wa kituo cha CDC cha Marekani Tom Frieden amesema, ingawa baadhi ya majimbo yamesitisha kuanzisha tena uchumi, lakini kwa kuwa ufanisi wa hatua za kinga utaonekana baada ya muda, idadi ya maambukizi ya Marekani huenda itaongezeka zaidi katika wiki kadhaa zijazo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako