• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yapanga kufungua uchumi huku ikiwa na tatizo la kuongezeka kwa wagonjwa wa COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-06-29 19:44:20

    Baadhi ya Wakenya wanatarajia serikali kufungua tena nchi Julai 6 kwa kuondoa zuio lililowekwa ili kukabiliana na kuenea kwa COVID-19.

    Hata hivyo mpango wa nchi kurudi katika hali ya kawaida unakabiliwa na changamoto wakati ambao maambukizi yanaongeza kwa kasi. Zuio lililowekwa ni pamoja na kuufunga mji wa Nairobi na Mombasa na amri ya kutotoka nje jioni hadi asubuhi. Baadhi ya biashara kama vile baa na shule na nyumba za ibada bado zinaendelea kufungwa huku magari ya abiria yakibeba nusu ya uwezo wake ili kukabiliana na kuenea kwa ugonjwa.

    Kenya ina matarajio kwamba rais Uhuru Kenyatta ataondoa zuio Julai 6 baada ya kufungua miji na kuondoa amri ya kutotoka nje. Kwenye mkutano wa Jumapili rais Kenyatta alisema zuio linaondoshwa ili kusaidia kukuza uchumi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako