• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Marekani haitafanikiwa kuchochea mzozo kati ya China na Afrika

  (GMT+08:00) 2020-06-29 21:17:06

  Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo hivi karibuni amedai China inaongeza mizigo ya madeni ya nchi za Afrika. Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Zhao Lijian amesema, kuchochea mzozo wa uhusiano kati ya China na Afrika ni kazi bure, na hakutafanikiwa.

  Pompeo tarehe 24 alitoa taarifa akilaani ahadi ya China kuzisaidia nchi za Afrika kukabiliana na janga la COVID-19, na kudai China ilificha ukweli wa maambukizi ya virusi vya Corona, na kuongeza mizigo ya madeni ya nchi za Afrika.

  Zhao amesema Pompeo anapuuza ukweli wa mambo, na kuipaka matope China bila ya msingi wowote. Amesema tangu kulipuka kwa virusi vya Corona, China imefuata msimamo wazi na kuwajibika, na kutoa habari kwa wakati kwa dunia nzima ikiwemo Marekani. Ameongeza kuwa, nchi za Afrika ni ndugu wakubwa wa China, na pande hizo mbili zimeshirikiana vizuri katika kupambana na virusi vya Corona.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako