• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatoa wito wa kuondoa vikwazo vya upande mmoja dhidi ya Syria

    (GMT+08:00) 2020-06-30 08:57:54

    Mjumbe wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Zhang Jun jana amezitaka nchi husika ziondoe vikwazo vya upande mmoja dhidi ya Syria, kutokana na hali mbaya ya kiuchumi na kibinadamu katika nchi hiyo.

    Balozi Zhang amesema, vikwazo vya upande mmoja ni sababu kuu ya msukosuko wa kiuchumi na kibinadamu nchini Syria.

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres ametoa wito wa kuondoa vikwazo ambavyo vimedhoofisha uwezo wa nchi katika kuzuia kuenea kwa janga la COVID-19. Vilevile ameliambaia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuwa, nchi za kikanda pia zimeeleza wasiwasi kuhusu vikwazo dhidi ya Syria, na kwamba vikwazo hivyo vimeathiri uchumi wa kanda hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako