• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Shule zafunguliwa nchini Tanzania huku tahadhari ikichukuliwa dhidi ya virusi vya Corona

  (GMT+08:00) 2020-06-30 09:10:30

  Shule nchini Tanzania ambazo zilifungwa na serikali Machi 17 ili kudhibiti kuenea kwa virusi vya Corona, zimefunguliwa hapo jana, huku hatua za tahadhari zikichukuliwa dhidi ya virusi hivyo.

  Shirika la Habari la China Xinhua lilishuhudia wanafunzi wamevaa barakoa na kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni, huku walimu wakihakikisha kuwa mwongozo wa kukinga na kuzuia virusi hivyo uliotolewa na mamlaka za afya unazingatiwa.

  Mwalimu mkuu wa Shule ya Sekondari ya Dodoma, Amani Mfaume amesema, uongozi wa shule hiyo umeamua kuwa utaendelea na masomo mpaka siku za Jumamosi ili kulipia muda uliopotea wakati wanafunzi walikuwa kwenye likizo ya miezi mitatu kutokana na mlipuko wa virusi vya Corona.

  Tarehe 17 mwezi huu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ilitoa mwongozo wa kufuatwa na shule ili kukinga maambukizi ya virusi hivyo, ikiwemo kuweka maeneo ya kunawa mikono na kuwataka wanafunzi wote kuvaa barakoa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako