• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • USAJILI: Timo Werner yuko tayari kuangusha saini kwenye timu tatu

  (GMT+08:00) 2020-06-30 16:40:40

  Nyota anayekipiga ndani ya Klabu ya RB Leipzig inayoshiriki Ligi Kuu ya nchini Ujerumani maarufu kama Bundesliga Timo Werner, amesema kuwa anaweza kusaini kwenye timu zote tatu ambazo zinahitaji saini yake kwa sasa iwapo mojawapo kati ya hizo itatimiza masharti yake. Miongoni mwa timu ambazo zinampigia hesabu nyota huyo ni pamoja na Chelsea ambayo inapewa nafasi kubwa ya kupata saini ya mshambuliaji huyo mwenye miaka 24. Mbali na Chelsea Inter Milan, Manchester United na Liverpool nazo pia zimeonyesha nia ya kupata saini ya nyota huyo ambaye anapenda kwenda kucheza ndani ya Ligi Kuu England. Mshambuliaji huyo amesema kuwa fedha kwake sio jambo la msingi ila anachotazama ni malengo ya timu kufika mbali na kutwaa mataji.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako