• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mamlaka za Marekani zaanza kuthibitisha tena ndege zake za Boeing 737 MAX

  (GMT+08:00) 2020-06-30 17:10:35

  Idara ya Usafiri wa Anga ya Marekani FAA imeanza majaribio ya safari za ndege zake za Boeing 737 MAX ili kuzithibitisha tena, ikiashiria hatua kubwa ya kurejea tena kwa ndege hizo kwenye huduma baada ya kuzuiliwa.

  Kwenye taarifa yake idara ya FAA imesema ndege ya Boeing 737 MAX iliondoka kwenye uwanja wa Boeing huko Seattle jimbo la Washington Marekani Jumatatu asubuhi kwa safari ya kwanza ya majaribio na kwamba idara pamoja na Boeing watafanya safari mfululizo za kuthibitisha tena wiki hii ili kutathmini mabadiliko yaliyopendekezwa na Boeing kwenye mfumo unaojiendesha wa kudhibiti safari kwenye 737 MAX.

  Wakati huohuo Shirika la Ndege la Norway limetangaza Jumatatu kuwa limefuta oda za ndege 97 za Boeing na litadai fidia kutoka kwa watengezaji hao wa Marekani kwa kuzuia ndge za 737 MAX na matatizo ya injini ya ndege za 787. Boeing imesema ipo kwenye mazungumzo na shirika hilo lililopo Oslo, kama inavyofanya na mashirika mengine ya ndege katika kipindi hiki wanachojitahidi kutimiza lengo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako