• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mazungumzo kuhusu mustakabali wa uhusiano kati ya Umoja wa Ulaya na Uingereza yaanza tena

  (GMT+08:00) 2020-06-30 17:16:09

  Mwakilishi wa kwanza wa mazungumzo wa Uingereza Bw. David Frost amewasili Brussels nchini Ubelgiji jana asubuhi kwa saa za huko na kukutana na mwakilishi wa kwanza wa Umoja wa Ulaya Bw. Michel Barnier na kuanza duru mpya ya mazungumzo kuhusu mustakabali wa uhusiano kati ya Umoja wa Ulaya na Uingereza. Hii ni mara ya kwanza kwa pande hizo mbili kufanya mawasiliano ya ana kwa ana tangu kutokea kwa janga la COVID-19.

  Kutokana na ajenda iliyotangazwa na kamati ya Umoja wa Ulaya, duru hiyo ya mazungumzo itafanyika kuanzia tarehe 29 mwezi Juni hadi tarehe 3 mwezi Julai, na mfumo wa mazungumzo hayo utapangwa na kuunganishwa vizuri ili pande hizo mbili zitilie maanani zaidi kuhusu masuala yaliyokwama.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako