• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wiki ya biashara ya kidijitali kati ya China na Afrika yafanyika kwa awamu ya kwanza

  (GMT+08:00) 2020-06-30 17:17:38

  Wiki ya biashara ya kidijitali kati ya China na Afrika inayofanyika kwa awamu ya kwanza imefunguliwa jana, ambapo mashirika ya kiserikali ya nchi 10 za Afrika yamehudhuria ufunguzi wa shughuli hiyo kwenye mtandao.

  Makampuni zaidi ya elfu moja ya China wanafanya biashara na wateja wa Afrika kwa kutumia njia ya video. Biashara hizo zinahusu vifaa vya ujenzi, nishati ya umeme, chakula, kilimo, matibabu ya familia na vifaa vya hotelini.

  Katika shughuli hizo za wiki moja, pande mbalimbali zitafanya mkutano wa baraza la biashara ya kidijitali kati ya China na Afrika katika mtandao, shughuli za kutanganza Kenya, Ghana na Morocco, na kuwaalika wataalamu kufafanua sera za Afrika na hali ya maendeleo ya uchumi na viwanda.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako