• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kampuni za China barani Afrika zaimarisha uzalishaji huku zikikabiliana na janga la COVID-19

  (GMT+08:00) 2020-06-30 17:18:57

  Hivi sasa maambukizi ya virusi vya Corona bado yanaendelea katika sehemu mbalimbali duniani zikiwemo nchi za Afrika. Kutokana na kukabiliwa na janga hilo, kampuni za China barani Afrika zimechukua hatua mbalimbali za kuhimiza uzalishaji, huku zikiimarisha hatua za kukinga virusi hivyo.

  Lamu iko katika pwani ya mashariki mwa Afrika, na miaka 600 iliyopita, ilikuwa kituo cha mwisho cha kikosi cha meli za China kilichoongozwa na Zheng He na kutembelea nusu ya dunia. Hivi sasa ujenzi wa mradi wa bandari ya Lamu ambao ni mradi muhimu wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja" unazidi kushika kasi. Baada ya kukamilika, bandari hiyo itakuwa njia kuu mpya ya baharini kwa nchi nyingi za Afrika Mashariki. Vituo kuanzia namba moja hadi3 vya meli vya bandari hiyo vinajengwa na Kampuni ya Ujenzi wa Mawasiliano ya Barabara ya China CCCC. Baada ya kutokea kwa mlipuko wa virusi vya Corona, namna ya kuendelea kusukuma mbele mradi huo wakati wa kukabiliana vizuri na virusi hivyo ilikuwa changamoto kubwa. Naibu meneja wa mradi huo wa kampuni ya CCCC Ou Liuhe anasema,

  "Tunatekeleza hatua maalumu wakati wa janga la COVID-19. Kila siku tunafuatilia hali ya maambukizi ya virusi vya Corona nchini China na Kenya, na kurekebisha nguvu ya kukinga virusi kufuatia hali ilivyo ya maambukizi. Kwa mfano tumefunga eneo la ujenzi, na kuwashawishi wafanyakazi wetu kuvaa barakoa, na kuwatahadharisha kudumisha umbali unaofaa wakati wa kuwasiliana."

  Nigeria ni nchi kubwa zaidi kwa uzalishaji wa mafuta barani Afrika. Kampuni ya Kemikali ya Mafuta ya China SINOPEC inatoa huduma katika visiwa viwili vya mafuta vya nchi hiyo. Naibu meneja mkuu wa tawi la kampuni hiyo nchini Nigeria Bw. Wan Guang amesema, wametunga mpango wa kukabiliana na maambukizi ya virusi vya Corona mapema sana. Anasema,

  "Kila siku idara ya usalama ya kampuni yetu inawapima joto wafanyakazi Wachina mara mbili. Pia tuna maofisa maalumu wanaowapima joto wafanyakazi na walinzi wa Nigeria, pamoja na washirika wetu. Mbali na hayo, tunatekeleza kwa makini utaratibu mkali wa kupokea wageni. Kama kuna wageni wanaotoka sehemu yenye maambukizi ya virusi vya Corona, haswa wale wenye homa, tunawaambia wasiingie kwenye eneo letu la uzalishaji, ili kuzuia virusi kutoka kwenye chanzo."

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako