• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mkuu wa jimbo la New York amtaka rais Trump kuvaa barakoa

  (GMT+08:00) 2020-06-30 19:14:32

  Mkuu wa jimbo la New York la Marekani Andrew Cuomo tarehe 29 alitangaza hali mpya za maambukizi ya virusi vya Corona kwenye mkutano na waandishi wa habari, na kumtaka rais Trump avae barakoa ili kuwa mfano wa kuigwa.

  Bw. Cuomo amesema, rais Trump anatakiwa kufanya mambo mawili, kwanza ni kusaini amri ya kuwataka watu wote kuvaa barakoa katika sehemu za umma, pili ni kuvaa barakoa ili kuwa mfano wa kuigwa.

  Bw. Cuomo ameitaka ikulu ya Marekani kutambua hali ya maambukizi ya virusi vya Corona na kuzingatia tishio la maambukizi. Amesema, kwa sasa kiongozi anapaswa kuwaambia Wamarekani ongezeko la maambukizi na hali nchini Marekani ikilinganishwa na nchi nyingine, ikiwemo hali ya uchumi ya Marekani, na kutambua hilo ndilo tishio halisi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako