• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Lionel Messi afikisha mabao 700, Barcelona wagawana pointi na Atletico Madrid

    (GMT+08:00) 2020-07-01 18:26:44

    Nyota wa ndani ya Klabu ya Barcelona Lionel Messi, usiku wa kuamika leo alifunga bao moja kwenye sare ya kufungana mabao 2-2 na Atletico Madrid Uwanja wa Nou Camp kwenye La Liga na kufikisha jumla ya mabao 700. Raia huyo wa Argentina anayekipiga pia kwenye timu ya taifa alifunga bao hilo kwa penalti iliyozama ndani ya nyavu na kumshinda mlinda mlango wa Atletico Madrid, Jan Oblak. Messi ametoka kwenye jumla ya mabao 699 aliyokuwa nayo kibindoni baada ya kufunga bao mbele ya Leganes wiki mbili zilizopita na alishindwa kufurukuta kwenye mechi tatu zilizopita ikiwa ni mbele ya Sevilla, Athletic Bilbao na Celta Vigo kabla ya kuibuka mbele ya Atletico na kufunga bao hilo. Nyota huyo mwenye miaka 33, anaongoza kwa kutupia jumla ya mabao 630 ndani ya Barcelona huku akitupia jumla ya mabao 70 kwenye timu yake ya taifa ya Argentina. Mabao ya Barcelona yalifungwa na Diego Costa dk 11 na Messi alifunga bao lake la 700 dk 50 kwa penalti. Yale ya Atletico Madrid yalifungwa na Saul Niguez dk 19 kwa penalti na dk 62 yote kwa penalti. Sare hiyo inawafanya Barcelona wagawane pointi mojamoja na wapinzani wakiwa nafasi ya pili na pointi 70 huku Real Madrid wakiwa nafasi ya kwanza na pointi 71.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako