• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kampuni za China nchini Jamhuri ya Watu wa Kongo zachangia juhudi za kukabiliana na COVID-19 nchini humo

    (GMT+08:00) 2020-07-02 19:11:22

    China na Jamhuri ya Watu wa Kongo zina urafiki mkubwa wa jadi. Tangu virusi vya Corona vilipuke nchini Jamhuri ya Watu wa Kongo mwezi Machi, serikali ya China imetoa misaada mbalimbali kwa nchi hiyo, wakati huohuo kampuni za China nchini humo pia zimetekeleza majukumu ya kijamii, na kushirikiana na watu wa nchi hiyo kukabiliana na maambukizi ya virusi hivyo.

    Tangu kutokea kwa mlipuko wa virusi vya Corona nchini Jamhuri ya Watu wa Kongo, serikali ya China imetoa aina mbalimbali ya misaada kwa nchi hiyo. Tarehe 15 Aprili, vifaa vya matibabu vilivyotolewa na China vilifikishwa nchini humo. Tarehe 23 Mei, kikundi cha wataalam wa China kilifika nchini humo ili kuisaidia kukabiliana na maambukizi ya virusi. Licha ya serikali, kampuni za China na Wachina walioko nchini humo pia wametoa misaada mbalimbali kwa nchi hiyo.

    Tawi la Kampuni ya Ujenzi ya China nchini Jamhuri ya Watu wa Kongo limejenga na linaendesha barabara ya No.1 mjini Brazzaville, ambayo inajulikana kama "Barabara ya Ndoto" kutokana na ubora wake wa juu. Naibu meneja mkuu wa tawi hilo Wang Shengli amesema, ili kukabiliana na virusi vya Corona, tawi hilo linachukua hatua kali kuhakikisha wafanyakazi wake wote hawaambukizwi virusi hivyo, huku ikiendelea na kazi za kawaida. Anasema,

    "Hatua zetu ni pamoja na kueneza elimu za kujikinga virusi vya Corona kabla ya kutokea kwa maambukizi, kutunga mpango wa kukabiliana na dharura, na mpango wa uzalishaji wakati wa maambukizi ya virusi hivyo. Hatua hizo zote zimetekelezwa kwa makini. Aidha, tunarekebisha kazi zetu kutokana na hali ilivyo ya maambukizi ya virusi hivyo, kama vile kupunguza au kusimamisha kazi, na kusimamisha kutuma wafanyakazi Wachina. Aidha, tumepanga sehemu ya kutengwa, na kuwaweka watu waliorudi kutoka nchi za nje karantini kwa siku 14."

    Tangu kutokea kwa mlipuko wa COVID-19, Jamhuri ya Watu wa Kongo imekabiliwa na upungufu wa vifaa vya kupambana na janga hili. Ingawa serikali ilichukua hatua mbalimbali zikiwemo kuwataka watu wote wasitoke kama hakuna ulazima, na kupiga marufuku ya kutotembea wakati wa usiku. Lakini baadhi ya watu dhaifu wakiwemo walemavu na mayatima bado wanakabiliwa na hatari kubwa, na kuhitaji misaada kutoka kwa jamii. Wang amesema tawi la Kampuni ya Ujenzi ya China nchini humo limetoa misaada mingi ya vifaa tiba na vitu vinavyohitajika maishani kwa Shirika la Walemavu Wanawake na nyumba tatu za mayatima. Licha ya hayo, lilichangia franc milioni tano za nchi hiyo kwenye mfuko wa kusaidiana.

    Tawi hilo lina wafanyakazi wenyeji wengi. Limewaandalia mafunzo kuhusu elimu za kukinga virusi vya Corona, na kuwapatia ruzuku ili kuwasaidia kushinda janga hilo.

    Kati ya wafanyakazi Wachina wa tawi hilo, kuna vijana wengi. Naibu meneja wa idara ya usimamizi wa jumla ya tawi hilo Yuan Jun ni mmojawapo. Anasema,

    "Sisi vijana tunafahamu zaidi mtandao wa Internet na vyombo vipya vya habari. Tunaweza kutoa mchango wetu maalumu."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako