• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya-Kaunti ya Mombasa yatenga Sh250milioni kuboresha sekta ya Uvuvi

    (GMT+08:00) 2020-07-02 19:27:52

    Serikali ya kaunti ya Mombasa,nchini Kenya imetenga Sh250m ili kuboresha sekta ya uvuvi katika kaunti hiyo.

    Kaunti ya Mombasa inalenga kutumia fedha hizo kuwanufaisha wavuvi kwa kununua maboti , kujenga vyumba vya kuhifadhi samaki, masoko ya kisasa na kutengeneza maeneo ya wavuvi kuweka vifaa vyao vya kazi na pia sehemu za kuegesha maboti yao.

    Kulingana na pendekezo la bajeti ya kaunti ya kipindi cha mwaka wa 2020/2021, serikali ya kaunti hiyo inayoongozwa na Gavana Hassan Joho, itatumia Sh120 milioni kununua maboti hayo, Sh80 milioni kujenga vyumba vya kuhifadhi samaki tani 100, wakati Sh20 milioni zitatumika kuweka soko la kisasa la samaki.

    Pendekezo hilo linasema kuwa mradi huo unakusudia kuongeza shughuli za uzalishaji wa samaki, kuhakikisha kaunti ina chakula cha kutosha na pia kutoa fursa zaidi za ajira kwa wanawake na vijana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako