• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Russia, Iran na Uturuki zasisitiza kuondoa vikwazo dhidi ya Syria

    (GMT+08:00) 2020-07-02 19:33:11

    Rais Hassan Rouhani wa Iran jana katika mkutano wa Astana kati ya viongozi wa Russia, Iran na Uturuki kwa njia ya video alisema kuwa, tangu kutokea kwa janga la COVID-19, watu wa Syria wamekuwa wanahitaji sana misaada ya kibinadamu, lakini Marekani ilmeiwekea Syria vikwazo, kitendo hicho ni ugaidi wa kiuchumi kwa watu wa Syria. Iran inalaani sana kitendo hicho na kusema itaendelea kutoa misaada kwa serikali na watu wa Syria.

    Rais Vladmir Putin wa Russia amesema, vikwazo vya Marekani dhidi ya Syria sio halali na vimezidisha hali mbaya nchini Syria. Ameongeza kuwa, ingawa mpango wa utatuzi wa suala la Syria haujatekelezwa, lakini kutokana na juhudi za Russia na Uturuki, wamepata mafanikio na suala la Syria litatatuliwa kwa njia ya kidiplomasia.

    Naye Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki amesema Uturuki itafanya juhudi zote kuhakikisha amani, usalama na utulivu wa Syria.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako