• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Timu 15 za utafiti kuhusu chanjo ya COVID-19 zatangaza mipango ya majaribio

  (GMT+08:00) 2020-07-03 09:21:54

  Mwanasayansi mwandamizi wa Shirika la Afya Duniani WHO Bibi Soumya Swaminathan amesema, katika Mkutano wa Pili wa Baraza la Utafiti na Uvumbuzi uliomalizika hivi karibuni, timu 15 za utafiti kuhusu chanjo ya COVID-19 zimetangaza mipango yao ya majaribio.

  Bibi. Swaminathan ameeleza kuwa, wanasayansi wote wameonesha hamu kubwa ya kufanya ushirikiano, na kufanya majadiliano ya kina kuhusu masuala ya utafiti, matibabu na chanjo katika kipindi kijacho.

  Mkurugenzi wa Idara ya utafiti na uendelezaji ya WHO Bibi Ana Maria Henao Restrepo amesema, ni vigumu kwa sasa kutangaza tarehe ya matumizi ya chanjo, lakini wanaharakisha hatua ya kufanya tathmini juu ya chanjo hizo na kufanya juhudi za kuongeza ufanisi wao.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako