• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Umoja wa Mataifa waonya athari za COVID-19 kwa amani na usalama

  (GMT+08:00) 2020-07-03 10:09:33
  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres amelikumbusha Baraza la Usalama la Umoja huo athari mbalimbali za virusi vya Corona kwa amani na usalama wa kimataifa.

  Akizungumza hapo jana, Katibu Mkuu huyo amesema janga la virusi vya Corona linaendelea kuathiri vibaya amani na utulivu duniani, na tishio lake ni la pande nyingi.

  Amesema matokeo yake yanaonekana hata katika nchi kadhaa ambazo kwa asili zilionekana kuwa tulivu, lakini athari zaidi iko wazi kwa nchi ambazo tayari zinashuhudia vita ama kumaliza vita.

  Bw. Guterres amesema, mivutano inaongezeka ikiwa ni matokeo ya kuvurugika kwa masuala ya kijamii na kiuchumi kutokana na janga hilo, uaminifu kwa taasisi unazidi kupungua katika maeneo ambayo watu wanafikiri kuwa mamlaka hazijakabiliana na janga hilo kwa ufanisi, ama haziko wazi kuhusu athari zake.

  Amesema nchi nyingi zimetakiwa kufanya tathmini jinsi zitakavyoendelea na uchaguzi uliopangwa kufanyika mwaka huu huku zikijaribu kudhibiti mgogoro wa kiafya.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako