• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yalitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kutafuta njia za kusimamisha mapigano duniani

  (GMT+08:00) 2020-07-03 10:10:30

  Balozi wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Zhang Jun amelitaka Baraza la Usalama la Umoja huo kutafuta suluhisho chanya la ombi la kusimamisha mapigano lililotolewa na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa ili kudhibiti janga la virusi vya Corona.

  Akizungumza kwenye mjadala wa ngazi ya juu kuhusu athari za virusi vya Corona, Balozi Zhang amesema, jamii ya kimataifa inapaswa kuchukua fursa hiyo kusaidia pande zinazopingana kujibu ombi hilo, kusimamisha mapigano mara moja, na kwa pamoja kupambana na janga la mlipuko wa virusi vya Corona.

  Amesema wakati Baraza hilo likipitisha azimio la ombi hilo, linapaswa kufanya kazi kuongeza kasi ya utekelezaji wake, na pia linapaswa kuongeza misaada ya kibinadamu na kufanya juhudi zaidi kuhakikisha ulinzi na usalama wa walinda amani.

  Balozi Zhang ameongeza kuwa, mshikamano na ushirikiano ni silaha kubwa katika kupambana na janga hilo, na China iko tayari kushirikiana na wadau wote, kusimamia msingi wa mfumo wa Umoja wa Mataifa na kuunga mkono nafasi ya uongozi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) katika mapambano dhidi ya virusi vya Corona.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako