• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yashuhudia wagonjwa wengi zaidi wa COVID-19 wakipona

    (GMT+08:00) 2020-07-03 18:42:58

    Jumla ya wagonjwa 60 wa COVID-19 wametibiwa hospitali na kuruhusiwa kurudi nyumbani katika wiki moja iliyopita hapa nchini China, ikiwa ni ongezeko la asilimia 46 kuliko katika wiki zilizopita.

    Kwenye mkutano na wanahabari, msemaji wa Idara ya Afya ya Taifa Hu Qiangqiang amesema wote kwa jumla walioruhusiwa kutoka hospitali baada ya kupona ni watu 78,499. Kulingana na ripoti ya kila siku kutoka idara hiyo, watu 12 waliruhusiwa kurudi nyumbani baada ya kupona jana Alhamis.

    Hu amesisitiza kuchukuliwa hatua zaidi za kawaida za kuzuia na kudhibiti, na kutoa wito wa kufanywa juhudi za kuboresha matibabu na tiba kwa wagonjwa wa COVID-19.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako