• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Waziri mkuu wa Ufaransa ajiuzulu

  (GMT+08:00) 2020-07-03 18:54:58

  Ikulu ya Ufaransa leo imetoa taarifa ikisema, rais Macron ameidhinisha barua ya kujiuzulu ya waziri mkuu wa nchi hiyo Edouard Philippe.

  Taarifa imesema Bw. Philippe na mawaziri wote wa serikali wataendelea kufanya kazi mpaka serikali mpya iundwe. Rais Macron amekubali na atateua waziri mkuu mpya ndani ya saa kadhaa.

  Habari kutoka televisheni ya BFMTV zinasema, mkutano wa mawaziri uliopangwa kufanyika asubuhi ya leo umefutwa.

  Habari nyingine zinasema, katika duru ya pili ya uchaguzi wa miji nchini Ufaransa, Bw. Philippe amechaguliwa meya wa mji wa Le Havre.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako