• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Vurugu za kufyatuliana risasi zashuhudiwa Chicago katika siku ya uhuru wikiendi hii

  (GMT+08:00) 2020-07-06 08:44:20

  Takriban watu 17 wameuawa na wengine 63 kujeruhiwa huko Chicago katika siku ya uhuru wikiendi hii kutokana na Vurugu za kufyatuliana risasi.

  Watu 17 waliouawa ni pamoja na watoto wawili, mmoja akiwa ni msichana mwenye miaka 7 na mwingine ni mvulana mwenye miaka 14. Kwa mujibu wa Chicago Tribune, hii ni wiki ya tatu mfululizo kushuhudia vifo vya watoto. Wikiendi iliyopita mtoto wa kiume mwenye umri wa miezi 20 na msichana mwenye miaka kumi waliuawa kwenye mashambulizi tofauti ya kufyatua risasi, na wiki moja kabla, watoto watano waliuawa kwa kupigwa risasi, akiwemo mvulana mwenye miaka mitatu.

  Mashambulizi mengi ya risasi yalitokea pande za Kusini na Magharibi, ambako ndio kuna vitendo vingi vya vurugu za kutumia silaha.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako