• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yatoa msaada wa vifaa tiba kwa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu

  (GMT+08:00) 2020-07-06 08:45:47

  Jumuiya ya Nchi za Kiarabu jana Jumapili imepokea msaada wa vifaa tiba uliotolewa na serikali ya China.

  Shehena hiyo ya msaada imekabidhiwa kwa maofisa wa jumuiya hiyo katika makao makuu yake mjini Cairo na balozi wa China nchini Misri Bw. Liao Liqiang.

  Balozi Liao amesema tangu virusi vya Corona vilipuke, China imetoa misaada mingi ya vifaa tiba kwa nchi za kiarabu, na pia kuzipatia uzoefu na teknolojia ya kupambana na virusi hivyo.

  Katibu mkuu msaidizi wa Jumuiya ya nchi za kiarabu Hossam Zaki ametoa shukrani kwa msaada wa kimatibabu wa China, na kusema huo unaonesha upeo na kina cha ushirikiano na urafiki kati ya jumuiya hiyo na China.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako