• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • 'TUNAWAJUA SIMBA, TUTAWAMALIZA' – Nahodha wa Yanga

    (GMT+08:00) 2020-07-06 17:21:10

    Wakati mechi ya michezo ya hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam Federation (FA) inakaribia nahodha wa Yanga, Juma Abdul, amewatoa hofu mashabiki wa Yanga na kuwataka kuwa na furaha kwenye kipindi hiki ambacho wanafanya maandalizi makubwa kuelekea kwenye mchezo dhidi ya watani wao wa jadi Simba. Yanga watacheza dhidi ya Simba kwenye, utakaofanyika Jumamosi ya mwishoni mwa wiki hii kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Abdul amesema timu hiyo inaendelea kujipanga kikamilifu kuwakabili Simba na kuwataka mashabiki wa Yanga waache kuwasikiliza wapinzani wao, kwani mbinu wanazopewa kwa sasa zinalenga kwenda kupata ushindi.

    Kwa sasa Yanga ambao wanaonekana kukosa kombe la ligi, wanakodolea macho Kombe la FA kama njia ya pekee ya kutafuta tiketi kuiwakilisha Tanzania kimataifa, ambako Simba tayari wametetea ubingwa wao kwa mara ya tatu mfululizo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako