• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wizara ya mambo ya nje ya China: Wanasiasa wa Marekani wapotosha ukweli wa mambo

  (GMT+08:00) 2020-07-06 20:11:59

  Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Zhao Lijian leo amesema, baadhi ya wanasiasa wa Marekani wamepotosha ukweli wa mambo na hata kutunga uongo, lengo lao ni kuidhalilisha China na WHO na kutaka kujinufaisha kisiasa. China inawataka waheshimu ukweli wa mambo na kuacha ujanja wa kisiasa.

  Hivi karibuni, Shirika la Afya Duniani WHO limerekebisha utaratibu wa kukabiliana virusi vya Corona. Mwenyekiti anayeshughulikia mambo ya China ya baraza la chini la bunge la Marekani Michael McCaul, ametoa taarifa akieleza mashaka yake kuhusu China kutangaza hali ya maambukizi kwa wakati na kwa uwazi.

  Bw. Zhao amesema kauli ya Marekani haiendani na ukweli wa mambo. China ilitangaza habari kuhusu maambukizi ya virusi kwa jumuiya ya kimataifa kwa wakati na kwa uwazi. Tarehe 31 Desemba mwaka jana, kamati ya afya ya mji wa Wuhan ilitoa taarifa kwenye tovuti yake kuhusu hali ya maambukizi ya nimonia. China mwanzoni kabisa ilitoa taarifa kwa WHO. Ukweli wa mambo uko wazi sana.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako