• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yasisitiza kuwa kuleta migongano kwenye uhusiano kati ya China na Afrika hakutaifanya Marekani iwe na uwezo mkubwa tena

    (GMT+08:00) 2020-07-10 19:04:17

    Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bw. Zhao Lijian amesisitiza kuwa kupaka matope ushirikiano kati ya China na Afrika, au kufanya uchochezi kwenye kati ya uhusiano wa pande hizo mbili hakutaweza "kuifanya Marekani iwe na uwezo mkubwa tena".

    Bw. Zhao amesema hayo baada ya waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bw. Mike Pompeo kusema Marekani inalalamikia ushirikiano kati ya China na Russia, na nchi za Afrika, ikizitaka nchi hizo za Afrika zitoe uamuzi na kutambua ukweli kwamba nchi za Ulaya na Marekani ni wenzi wao kihalisi wa ushirikiano, na kwamba Marekani inatoa msaada wa kibinadamu kwa nchi za Afrika kutokana na kuwa hii ni sera sahihi, na lengo la China la kutoa msaada ni kujipatia faida.

    Kutokana na kauli hiyo Bw. Zhao amesema China imetoa misaada mingi ya vifaa kuzisaidia nchi za Afrika kupambana na virusi vya Corona, pia inashirikiana na jumuiya ya kimataifa kuongeza misaada kwa nchi za Afrika na kupunguza mzigo wao wa madeni. Pia amesisitiza kuwa ushirikiano kati ya China na Afrika uko wazi, na unakaribisha ufuatiliaji na uwekezaji kutoka kwa jumuiya ya kimataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako