• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • CHESS: Kocha wa Chess avutiwa na shindano la vijana wadogo la Afrika

    (GMT+08:00) 2020-07-13 15:45:33

    Kocha wa mchezo wa Chess nchini Tanzania, Kara Louis ameelezea mashindano ya mchezo huo yaliyofanyika kwa njia ya mtandao yajulikanayo kama African Juniors 11 Team Battle yaliyohusisha nchi sita, kuwa ni mashindano mazuri yatakayowatangaza wachezaji wadogo. Louis amesema hayo jana kando ya mashindano hayo yaliyoshirikisha wachezaji kutoka nchi mwenyeji Tanzania, Uganda, Zimbabwe, Afrika Kusini, Malawi na Botswana. Miezi michache iliyopita, kutokana na kuzuiwa kwa shughuli zote za michezo ili kudhibiti kuenea kwa maambukizi ya virusi vya Corona, Shirikisho la Chess Tanzania lilitangaza kuwa litaanzisha mashindano kwa njia ya mtandao yatakayojumuisha wachezaji wa umri wote.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako