• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Manchester City waponea adhabu baada ya CAS kubatilisha maamuzi ya UEFA

    (GMT+08:00) 2020-07-14 16:04:02

    Imekuwa afueni kubwa kwa Manchester City baada ya Mahakama ya Kimataifa ya Migogoro katika Michezo (CAS) kubatilisha maamuzi ya awali ya UEFA ambao wamewapiga miamba hao wa soka Uingereza marufuku ya kushiriki kipute cha Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) kwa kipindi cha misimu miwili. Kwa mujibu wa CAS, hakuna ushahidi wa kutosha wa kuthibitisha matumizi mabaya ya fedha kambini mwa kikosi cha Man-City. Februari mwaka huu Bodi ya UEFA inayodhibiti matumizi ya fedha miongoni mwa klabu za bara Ulaya (CFCB) iliwaadhibu Man-City kwa kukiuka kanuni za matumizi ya fedha (FFP) kati ya mwaka 2012 na 2016, pia walidai kuwa Man-City walikataa kushirikiana vilivyo na vinara wa Uefa waliokuwa wakiwachunguza kuhusiana na kesi hiyo. Hata hivyo, Afisa Mkuu Mtendaji wa Man-City, Ferran Soriano alikana madai hayo na kukata rufaa na kesi hiyo ikasikilizwa na mawakili watatu wa CAS kupitia njia ya video za siri kati ya Juni 8-10, 2020.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako