• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Huawei yasema hatua ya Uingereza kuipiga marufuku kampuni hiyo itarudisha nyuma maendeleo ya kidigitali

    (GMT+08:00) 2020-07-15 09:28:05

    Kampuni ya Huawei ya China imesema uamuzi wa serikali ya Uingereza kuipiga marufuku kampuni hiyo kushiriki kwenye utengenezaji wa mtandao wa 5G 'ni wa kukatisha tamaa' na unatishia 'kupunguza kasi ya maendeleo ya kidigitali ya Uingereza, kufanya gharama za huduma ziwe juu na kuongeza pengo la kidigitali.'

    Msemaji wa kampuni ya Huawei nchini Uingereza Bw. Ed Brewster amesema huu ni uamuzi wa kusikitisha na ni habari mbaya kwa kila mtu mwenye simu ya mkononi nchini Uingereza.

    Jana serikali ya Uingereza ilitangaza kuwa kununua vifaa vya 5G kutapigwa marufuku kuanzia tarehe 31 Desemba mwaka huu, na vifaa vyote vya kampuni ya Huawei vya teknolojia ya 5G nchini Uingereza vitaondolewa kabla ya mwisho wa mwaka 2027.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako