• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Harry Kane apitisha idadi ya mabao 200 akicheza soka katika kiwango cha klabu

    (GMT+08:00) 2020-07-16 16:07:23

    Mshambuliaji Harry Kane alifikisha zaidi ya mabao 200 katika taaluma yake ya soka kwenye ngazi ya klabu baada ya kutikisa wavu mara moja na kusaidia Tottenham Hotspur kuwapepeta Newcastle United 3-1 katika Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) hapo jana. Matokeo hayo yaliweka hai matumaini ya Tottenham ya kushiriki soka ya bara Ulaya (Europa League) msimu ujao wa 2020-21. Hii ni baada ya wachezaji hao wa kocha Jose Mourinho kupaa hadi nafasi ya saba kwa alama 55 kwenye msimamo wa jedwali la EPL. Nahodha huyo wa Tottenham na timu ya taifa ya Uingereza, alipachika wavuni bao lake la 201 mwishoni mwa kipindi cha pili baada ya kuuwahi mpira uliotemwa na kipa Martin Dubravka kutokana na fataki ya Erik Lamela.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako