• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping aeleza imani yake kwa uchumi wa China na kuahidi kufungua zaidi mlango

    (GMT+08:00) 2020-07-16 16:35:01

    Rais Xi Jinping wa China amesema msingi wa ukuaji mzuri wa uchumi wa China kwa muda mrefu haujabadilika na hautabadilika.

    Rais Xi amesema hayo alipojibu barua iliyoandikwa na wawakilishi wa Baraza la Watendaji Wakuu wa Makampuni Duniani, na kuahidi kuwa China itaendelea kufanya mageuzi ya kina na kufungua mlango zaidi, pia kuweka mazingira mazuri ya kibiashara kwa uwekezaji na maendeleo ya kampuni za ndani na nje ya China.

    Amesema China inakabiliana na virusi vya Corona na maendeleo ya uchumi na jamii kwa kufuata utaratibu sahihi, ikitaka kujenga jamii yenye ustawi wa kati katika nyanja zote na kutokomeza umasikini.

    Katika barua yao, wajumbe wa Baraza la Watendaji Wakuu wa Makampuni Duniani waliisifu China, chini ya uongozi imara wa rais Xi Jinping, imefanikiwa kudhibiti janga la virusi vya Corona, kuchukua nafasi ya uongozi katika kurejesha shughuli za kibiashara na uzalishaji mali, na kuchukua nafasi chanya katika kuunga mkono mapambano ya dunia dhidi ya virusi vya Corona na kudumisha utulivu wa uchumi wa dunia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako