• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Benki ya Stanbic Tanzania yaunda kaulimbiu mpya "Inawezekana"

  (GMT+08:00) 2020-07-16 19:46:37

  Benki ya Stanbic Tanzania imesema siri ya kukua kibiashara imetokana na maendeleo ya wateja wake na wananchi kwa ujumla.

  Mkurugenzi Mkuu wa benki hiyo nchini, Kevin Wingfield alisema hatua hiyo imewapa motisha ya kuunda kauli mbiu mpya ya 'Inawezekana' ambayo inafanana na nafasi yake katika jamii.

  Wingfield alisema kuwa wakiwa kwenye Maadhimisho ya miaka 25 tangu kuanzishwa kwa benki hiyo nchini Tanzania, wamefanya tathmini na kugundua maendeleo ya benki yao katika kukua kibiashara yamechagizwa na maendeleo ya wateja wao na wananchi,hivyo wakachochewa kuja na kauli mbiu inayokwenda sambamba na ukuaji wa benki yao.

  Alisema kaulimbibu hiyo inaakisi benki hiyo imekua, inavyoendelea kukua kutokana na huduma bora wanazotoa kwa wateja na mtazamo wa wateja wao na fursa zilizopo. Alisema benki yake inaamini ndoto ni chachu ya maendeleo, hivyo ni lazima benki hiyo na wateja wake kwa pamoja kuwa tayari kuchukua hatua mpya ili kufanikisha ndoto zao hizo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako