• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kufungua majumba ya sinema wakati janga la virusi vya Corona likipungua

    (GMT+08:00) 2020-07-16 19:52:36

    Idara ya Filamu nchini China imetangaza kuwa, majumba ya sinema katika maeneo yaliyo kwenye hatari ya chini yatafunguliwa tena kuanzia Julai 20 kutokana na mafanikio katika kudhibiti janga la virusi vya Corona.

    Idara hiyo imesema, majumba hayo ya sinema yanapaswa kufunguliwa tena kwenye maeneo ambayo hatua za kukinga na kudhibiti virusi zimetekelezwa, na kwamba majumba hayo yanapaswa kusimamisha shughuli zao mara maeneo yao yatakapobadilishwa na kuwekwa kwenye hatari ya kati au ya juu.

    Pia Idara hiyo imeelekeza kuwa, idadi ya watu haipaswi kuzidi asilimia 30, na watu wanaotaka kwenda kutazama filamu wanapaswa kuweka miadi mapema kwa kutumia majina yao halisi na kununua tiketi kupitia mtandao.

    Idara hiyo imesema, watu wasiovaa barakoa na wale ambao joto lao la mwili litazidi nyuzi 37.3 hawataruhusiwa kuingia kwenye majumba hayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako