• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Ushirika kuzalisha miche mingi ya kahawa

  (GMT+08:00) 2020-07-17 19:33:59

  Chama Kikuu cha Ushirika Mbinga (MBIFACU),kimesema katika msimu huu imepanda miche ya kisasa ya kahawa 23,275.Kaimu Meneja wa Henrick Ndimbo amesema kuwa ifikapo mwaka 2023 wanatarajia kuzalisha kahawa tani zaidi ya 23,000 ambazo zitawaingizia Sh. milioni 69 na kuongeza mapato ndani ya chama.

  Akizungumzia historia ya shamba hilo, Ndimbo alisema katika kijiji cha Ugano, wanamiliki eneo la hekari 1,052 na kwamba bado wana shamba la zamani la kahawa lenye ukubwa wa hekari 50.

  Alisema walipokabidhiwa miche hiyo kutoka kwa Chama Kikuu cha Ushirika cha MBICU, waliamua kuifufua upya miche hiyo na kuacha baadhi ya miche ya zamani inayotumika kama shamba darasa.

  Naye Kaimu Makamu Mwenyekiti wa MBIFACU, Winfred Lupembe, alisema shamba hilo litaimairisha uchumi wa chama hicho. Alisema katika shamba jipya, miche ya kahawa imefunikwa kwa majani ili kuilinda wakati wa baridi na wakati wa jua kali isipate mwanga mkali na kuathirika.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako