• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Viongozi Magharibi wamtaka Rais atimize ahadi ya kufufua sekta ya sukari

    (GMT+08:00) 2020-07-17 19:34:25

    Viongozi nchini Kenya wameitaka serikali kufadhili mpango wa ustawishaji kilimo cha miwa kufufua sekta hiyo inayokabiliwa na changamoto nyingi.

    Viongozi hao wameitaka serikali kuwekeza fedha katika shughuli ya utafiti wa miwa ili kuimarisha uzalishaji wa zao hilo.

    Wameongeza kuwa ili kufufua sekta ya sukari nchini Kenya, serikali ianze kufadhili shughuli kama utafiti ili kuwezesha viwanda vya Kenya kupata malighafi tosha. Wanasema hatua ya kufutilia mbali mzigo wa madeni kwa viwanda vinavyomilikiwa na serikali haitasaidia zaidi ikiwa kiwango cha uzalishaji miwa nchini Kenya kitasalia chini.

    Wamesisistiza kuwa wangependa kuona trekta zikilima mashamba kwa ajili ya uzalishaji miwa lakini jambo muhimu zaidi ni kufadhili utafiti kando na kukarabati mashine kuukuu katika viwanda vya miwa.

    Aidha viongozi hao wamesema kile wangependa kuona ni suluhu la kudumu kwa changamoto inayowakabili wakulima wa miwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako