• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • KPC yatangaza hasara ya shilingi bilioni 2.8

    (GMT+08:00) 2020-07-17 19:34:45

    Shirika la bomba la mafuta nchini Kenya Kenya Pipeline Company limetangaza hasara ya shilingi bilioni 2.8 ndani ya kipindi cha miezi mitatu kutokana na kupungua kwa mahitajhi ya bidhaa hiyo. Kampuni hiyo imesema baadhi ya mambo ambayo yamesababisha hali hiyo ni kusitishwa kwa safari za ndege pamoja na marufuku za kutotoka nje ambazo zimewekwa na serikali kwa kipindi Fulani. Imesema marufuku hiyo imefanya watu wengi kukosa kusafiri hali ambayo imechangia kwa kupungua kwa uuzaji wa mafuta na hatimaye kupunguza usafirishaji wa mafuta kwa kutumia mabomba kwa asilimia 40. Katibu mkuu mtendaji wa KPC Bw Irungu Macharia, amesema tayari shirika hilo limesitisha huifadhi wa mafuta katika hazina zake za Nakuru na Mombasa ikiwa ni njia ya kuzuia maambukizi ya virusi vya Corona.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako