• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wizara yatoa mafunzo kwa wachuna ngozi 700

  (GMT+08:00) 2020-07-17 19:35:06

  Wizara ya Mifugo na Uvuvi Tanzania hadi kufikia sasa imetoa mafunzo kwa wachunaji wa ngozi za wanyama takriban 735 nchini humo.

  Mkurugenzi Msaidizi wa Mazao ya Mifugo, Usalama wa Chakula na Lishe, Gabriel Bura, amesema hatua hiyo ni jitihada za kuhakikisha kuwa thamani ya ngozi inaongezeka nchini Tanzania. Bura alisema kuwa mafunzo hayo yametolewa katika mikoa ya Kilimanjaro, Manyara, Arusha, Mwanza, Simiyu, Shinyanga, Morogoro na Kagera, huku akiongeza kuwa mchakato wa kutoa leseni kwenye mikoa hiyo umeshaanza.

  Aidha ameongeza kuwa wameanza kugawa visu vinavyotakiwa kitaalamu kwa ajili ya kazi ya uchunaji katika mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara na mchakato wa kuhakikisha vinafika katika kanda zote walizotoa mafunzo.

  Aliongeza kuwa hatua inayosubiriwa ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi kusaini nyaraka za uteuzi wa wakaguzi wa ngozi waliopatikana kutoka kwenye Halmashauri 113 ambao tayari wameshapitishwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali na baada ya taratibu kukamilika, wataalamu hao watakuwa na jukumu la kuhakikisha wanasimamia ubora wa ngozi kama walivyoainishwa kwenye Sheria Namba 18 ya Masuala ya Ngozi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako