• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wafanyibiashara wa chini na kati kupitia wakati mgumu kwa miezi sita ijayo.

  (GMT+08:00) 2020-07-20 15:39:15

  Huku virusi vya corona vikizidi kuenea nchini Kenya, utafiti wa hivi punde unaonyesha kwamba wafanyibiashara wa chini na wale wa kiwango cha wastan watapitia wakati mgumu sana miezi sita ijayo. Hii ni kutokana na wasiwasi walio nao wafanyibiashara hawa, kutokana na makali ya virusi vya corona.

  Utafiti uliofanywa na mashirika matatu ya utafitiā€¦.SNDBX village, Wylde International na Amethyst Consulting, unaonyesha kwamba asilimia 54 ya wafanyibiashara hawa wa kiwango cha chini na wastan wanatarajia kupungua kwa fedha na mauzo .

  Asiliamia 68 ya waliohojiwa wanasema kwamba biashara ilikuwa ya chini mno mwezi wa Aprili ikilinganishwa na mwezi Machi wakati Kenya iliweka amri ya kutokuwa nje, kufungwa kwa shule, maeneo ya burudani na masharti mengine kama njia za kupunguza kuenea kwa virusi vya corona.

  Aidha utafiti huo pia unaonyesha kwamba asilimia 26 ya wafanyibiashara hawa wanapata ugumu sana kuwalipa wafanyikazi wao. Asilimia 19 wanatarajia kushuhudia hasara huku asilimia 19 nyingine wakisema kwamba watapata ugumu kulipa mikopo yao.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako