• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Watalii 270 watua Zanzibar

  (GMT+08:00) 2020-07-20 15:39:44

  Watalii 273 waliingia nchini Zanzibar mwezi uliopita, baada ya sekta hiyo kuanza kurejea kufuatia kupungua kwa maambukizi ya corona na kurejeshwa kwa huduma za usafiri wa anga.

  Mtakwimu Kitengo cha Utalii Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Raya Mohammed Mahfoudh, aliyasema hayo wikendi hii ambayo imepita alipowasilisha takwimu za uingiaji wa wageni nchini humo.

  Alisema idadi hiyo ya wageni imeongezeka kulinganishwa na wageni 173, walioingia Zanzibara mwezi Mei mwaka huu. Alibainisha kuwa asilimia 48.4 ya wageni hao walitoka Ulaya.

  Alisema asilimia 52 ya wageni hao walipitia uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume na asilimia 48 walipitia bandarini.

  Vile vile, asilimia 52.4 ya wageni ni wanaume na 47.6 ni wanawake. Wadadisi wanasema kwamba kurejea kwa sekta ya utalii ni faraja kwa maendeleo ya uchumi wa Zanzibara, baada ya zuio la takriban miezi minne, lililosababisha sekta hiyo kuyumba kwa kiasi kikubwa.

  Sekta ya utalii huenda ikapigwa jeki hivi karibuni baada ya hali kuwa nafuu Italia, ambalo hutoa idadi kubwa ya wageni wanaokuja Zanzibar.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako