• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tanzania: Serikali yatambua mchango wa wadau wa kilimo uchumi wa kati

  (GMT+08:00) 2020-07-20 15:40:18

  Serikali imesema inatambua mchango wa wadau binafsi katika kukuza na kuendeleza sekta ya kilimo nchini, na kuwa sehemu ya mchango wa kuiwezesha Tanzania kufikia uchumi wa kati.

  Hayo yalisemwa mwishoni mwa wiki jana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Gerald Kusaya, alipoitembelea kampuni ya uuzaji wa zana za Kilimo ya Agricom Africa Ltd, iliyopo Kata ya Igurusi, Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya.

  Kusaya alisema kampuni hiyo imekuwa na mchango mkubwa katika kuwawezesha wakulima nyenzo za kilimo, yakiwamo matrekta, pawatila na mashine zinazotumika kuvuna mpunga, pamoja na kutoa elimu ya kufanya kilimo bora chenye tija.

  Alisema kuwa sekta ya kilimo ndiyo inayoongoza kwa kutoa ajira nchini Tanzania, hivyo imekuwa sehemu ya kuchnagia pato la taifa nchini, kutokana na rasilimali zinazozalishwa kutumika kwa ajili ya shughuli za biashara pamoja na kilimo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako